Bill Nass amefunguka hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Hatua Tatu ndani ya TimesFm ambapo amesema kwa sasa anafahamika kwa wadau kutokana na ngoma yake ya Raha aliyomshiriksha Naziz na T.I.D huku pia aliweza kupata nafasi ya kuchaguliwa kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro.
“Ngoma ile imenibariki sana, nimefanikiwa kiasi flani kutengeneza jukwaa la kujulikana kwa watu na sasa nimeshaachia ngoma mpya inayoitwa Ligi Ndogo ambayo pia imepokelewa vizuri”, alieleza Bill Nass.
Bill Nass naye ni moja kati ya Wasanii watakao panda jukwaani jumamosi 29.08.2015 pale Dar Live kwenye fainal za shindano la HipHop “The Jump Off Michano” lililoandaliwa na radio ya timesfm.
No comments:
Post a Comment