Saturday, 29 August 2015

Madai Mtoto si wa Diamond, Zari Aitwa Kwao Uganda

                                             
KIMENUKA! Baada ya madai kwamba mtoto Latifah ‘Tiffah’ si damu ya Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku shemeji wa zamani wa Zarinah Hassan ‘Zari’ (mama Tiffah), King Lawrence naye kusema mtoto huyo ni wake, kuna taarifa mpya zinazodai kuwa, Zari ameitwa kwao, Uganda ili akamalize ubishi juu ya suala hilo, Risasi Jumamosi limenasa mchapo kamili.
Hivi karibuni baada ya Zari kujifungua, King Lawrence alijitokeza na kudai kuwa, mtoto huyo ni wake na kusema kama kuna anayebisha kiitishwe kipimo cha vinasaba (DNA), hivyo kuibua mkanganyiko na taarifa zilizozagaa awali kuwa, mtoto huyo ni wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni, Zari alipigiwa simu na mama yake mzazi, Halima Hassan akimtaka aende nyumbani kwao ili akawaeleze ukweli ndugu zake ambao wamekuwa njia panda baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba Tiffah si wa Diamond ambaye familia inamtambua kwa sasa.
“Taarifa zinawafikia tofauti. Kuna zile za awali kwamba mtoto huyo ni wa Ivan, mara zikaibuka nyingine kwamba ni wa King Lawrence hivyo mama amemuita Zari ili akategue kitendawili hicho kumaliza ubishi.

ATAKIWA KWENDA NA UKWELI
“Amemtaka aende na ukweli moyoni maana yeye (Zari) ndiye anayeujua. Hata hiyo DNA haina maana. Ameambiwa kwamba siku zote mama ndiye anayejua ukweli wa mtoto ni wa nani,” kilisema chanzo hicho.

ATAKIWA AMUOGOPE MUNGU
Chanzo kilizidi kunyetisha kuwa, mbali na kumtaka aende na ukweli, familia imemtahadharisha atakapofika aseme ukweli kwa kumuogopa Mungu maana vinginevyo dhambi hiyo itamhukumu maisha yake yote.
“Ametahadharishwa na familia kwamba anapaswa kumuogopa Mungu maana ni dhambi mtoto wa baba huyu kumpa baba huyu. Wao Kama familia wanajua Tiffah ni wa Diamond. Sasa wanakangaywa na hao wanaodai wao ndiyo haswa wahusika.

HAWAHOFII KAMA SI WA DIAMOND
“Familia imesema haina shida hata kama itakuwa mtoto si wa Diamond lakini wanachotaka wao ni kujua ukweli tu.” Chanzo.

DIAMOND ANASEMAJE?
Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu hivi karibuni baada ya King Lawrence kuibuka na barua ya wakili kuitisha kipimo cha DNA akidai mtoto ni wake, Diamond alisisitiza kwamba mtoto huyo ni damu yake hivyo hana muda wa kubishana na mtu.

“Huyo jamaa (King Lawrence) atakuwa anatafuta kiki katika vyombo vya habari. Huyohuyo ndiye alianza kusema mtoto si wangu ni wa Ivan mara amegeuka tena na kusema ni wake yeye, hata haeleweki. Siwezi kujibishana naye.
“Hata hiyo barua aliyosema ni ya wakili ya kutaka DNA, haijatufikia! Nasikia tu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,” alisema Diamond.

KUHUSU SAFARI
Alipotafutwa Diamond ili aeleze kuhusu taarifa za mama Tiffah kuitwa nchini Uganda ili akaeleze ukweli, alisema hayo ni mambo ya kifamilia zaidi na hata hivyo haoni tatizo ndugu kumwita Zari kwani ukweli Tiffah ni damu yake na hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea.
“Tiffah ni damu yangu hata akienda hakuna kitakachobadilika. Sina wasiwasi maana mimi najua mahesabu yake yote na ninajua mpaka tarehe niliyokutana naye na mtoto akawepo,” alisema Diamond huku akisema, Zari hana nafasi ya kuongea na vyombo vya habari.

NCHINI UGANDA
Nchini Uganda, bado baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti mkanganyiko wa mtoto wa Diamond ambapo baadhi ya magazeti yametaka Zari aende akapime DNA ili kujiridhisha kuhusu uhalisia.

AFRIKA KUSINI
Nazo habari kutoka nchini Afrika Kusini ambako ndiko kwenye makazi ya Zari, baadhi ya Wabongo wanaoishi jirani na Zari walisema wanatambua uwepo wa Diamond kama mpenzi mpya wa Zari kwa hiyo hakuna shaka kuwa yeye ndiye baba (biological father) wa Tiffah.
Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya simu juzi, mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Steve, alisema amekuwa akimfuatilia kwa karibu King Lawrence kupitia Instagram yake akidai kwamba yeye ni baba wa Tiffah, lakini sehemu kubwa ya watu wenye ujirani na Zari kule wanaamini, Diamond ndiye baba husika.

“Kuhusu Diamond kuwa baba wa Latifah hilo halina ubishi. Hata sisi huku tunajua hivyo. Hili suala liangaliwe kwa macho matatu. Nahisi kuna ‘vita’ ya sisi Watanzania na Waganda kuhusu mtoto,” alisema Mbongo huyo.

No comments:

Post a Comment