Mahakama ya Misri imewahukumu waandishi watatu wa kituo cha runinga cha
Al jazeera kwenda jela miaka mitatu.
Hukumu hiyo ilitolewa baada ya waandishi hao
Mohamed Fahmy, Peter Greste na Baher Mohamed kupatikana na hatia ya kutangaza habari za uongo na kulisaidia kundi la
Muslim Brotherhood ambalo kwa sasa linatambuliwa kama kundi la kigaidi.
Baher Mohamed pia alihukumiwa kifungo kingine cha miezi sita.
Hata hivyo mmoja wa waandishi hao
Peter Greste, yuko nje ya nchi hiyo baada ya kutimuliwa kutoka nchini kwake tangu mwezi Ferbruari.
No comments:
Post a Comment