Mratibu
wa Mashindano ya Mechi ya Boda boda kutoka Mashujaa FM Radio 89.3 Lindi
akiwa na Vifaa vya Michezo ambavyo vimekabidhiwa kwa Viongozi wa timu
za Madereva Boda Boda wa Manispaa ya Lindi ambapo Madereva wa Standi
watawavaa madereva wa Soko Kuu Lindi.
Kiongozi
wa Madereva Boda Boda wa Stand akipokea jozi ya Jezi tayari kabisa kwa
Mchezo wa Kesho dhidi ya wale wa Soko Kuu Lindi. Aliyekabidhi Jezi hizo
ni Mohamed Mustafa (Mratibu wa Mchezo huo kutoka Mashujaa FM)
Kiongozi
wa Madereva Boda Boda wa Soko Kuu Lindi akipokea jozi ya Jezi tayari
kabisa kwa Mchezo wa Kesho dhidi ya wale wa Standi Lindi. Aliyekabidhi
Jezi hizo ni Mohamed Mustafa (Mratibu wa Mchezo huo kutoka Mashujaa FM)
Viongozi na waamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu utakao fanyika leo tarehe 29/8/2015 kati ya Madereva Bodaboda wa Standi na Sokoni ulio andaliwa na Mashujaa Fm Redio. Leo Timu hizo zimekabidhiwa vifaa vya kimichezo kama vile Jezi na Mpira ambavyo vitatumika siku ya kesho.
Viongozi kutoka pande zote mbili wamekabidhiwa jezi jozi moja kila upande ambazo zitatumika katika mpambano huo utakao fanyika siku ya kesho katika viwanja vya Ilulu uliopo Manispaa ya Lindi.
Saidi Tayari ni kiongozi wa timu ya bodaboda kutoka Sokoni ameahidi ushindi mmono siku ya kesho dhidi ya maasimu wao bodaboda wa standi wazee watoroka uje. Kwa upande wa kiongozi kutoka standi Shaweji Ateta amejinasibu kua ushindi ni lazima kwa upande wao maana wamejipanga zaidi amewataka maasimu wake wajiandae kupokea mvua ya magoli.
Katika kikao hicho wamekubaliana kuto kuchezesha mamluki katika mchezo huo kwani wanaotakiwa kucheza mchezo huo ni madereva wa boda boda na si vinginevyo.
Kwa upande wake Mratibu wa mashindano hayo Mudy Muzungu kutoka Mashujaa Fm Redio amesema maandalizi yamekamilika kinacho subiriwa ni siku ya kesho kupigwa kwa mtanange huo.
Muzungu amefafanua kua mshindi katika mchezo huo atapata kikombe na katika mchezo huo mgeni rasmi ni Kamanda wapolisi mkoa walindi na mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 10 jioni siku ya leo jumamosi katika viwanja vya Ilulu.
No comments:
Post a Comment