KUFUATIA kuwepo kwa madai na minong’ono
mingi ya msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel kumzidi umri mzazi
mwenzake, Moses Iyobo, muigizaji huyo ‘amewaka’ na kuwataka watu
wasiingilie uhusiano wao na kwamba suala la umri kwao ni namba tu.
‘Akibananishwa ukutani’ na mwandishi
wetu kwa maswali magumu hivi karibuni, Aunt alisema amekuwa akiumizwa na
maneno yanayoendelea juu ya kumzidi umri Iyobo, na kusema hayuko tayari
kuona uhusiano huo ukivunjwa kwa maneno ya aliowaita “wakosa kazi”.
“Kwani wakati tunatongozana hatukujua
kuwa tunazidiana umri? Mbona watu wanashindwa kufanya mambo ya msingi na
kukalia majungu? Kwetu sisi suala la umri ni namba tu, labda nikuulize,
ulishaona mtoto anambebesha mwanamke mimba? Maneno ya mimi kumzidi umri
Iyobo yananiumiza sana kwa kweli, lakini nitaulinda uhusiano huu hadi
mwisho,” alisema Aunt Ezekiel
No comments:
Post a Comment