Monday, 7 September 2015

Nimetumwa na wananchi naamini watanipokea-Roma

           
 Rapa ambaye siku zote amekuwa akiwatetea wanyonge kupitia muziki wake Roma Mkatoliki amefunguka na kusema katika kazi yake mpya amezungumza mambo mengi zaidi ya kazi zake zote za alizofanya hapo awali.
 
 
Roma Mkatoliki amesema haya katika kipindi cha Planet Bongo na kudai anawasiwasi huenda kazi hiyo isipate nafasi katika baadhi ya vituo vya radio kutokana na maudhui yake japo anaamini moja kwa moja kazi hiyo itafanya vizuri mtaani sababu inazungumzia uhalisia wa maisha ya watanzania na siasa za Tanzania.
Katika hatua nyingine Roma amesema kwa sasa wasanii wengi wanaogopa kuachia nyimbo zao kwa sababu ya siasa na kuona wanaweza wasipate nafasi ya kutosha katika vyombo vya habari kutokana na jamii kuegemea sana katika masuala ya siasa.
"Kwa sasa wasanii wengi wanaogopa kutoa nyimbo wakihisi kutopata nafasi kutokana na masuala ya siasa lakini kwangu mimi ni lazima nitoe wimbo huo tarehe 9 ya mwezi huu sababu kwanza niliahidi kutoa wimbo mwaka huu, lakini pia wimbo huu nimetumwa na wananchi nizungumze haya kabla ya wao kufanyika uchaguzi Oktoba 25, na humu nimezungumzia siasa kiujumla ila wimbo haujaegemea katika chama fulani ila ni masuala ya siasa," alisema Roma Mkatoliki.
Msanii huyo anakiri wazi kuwa kila aliyepata kusikiliza wimbo huo aliondoka na swali na wengi wao walionyesha hali ya kuogopa kutokana na kile alichozungumza katika wimbo huo ambao umepewa jina la "Viva Roma Viva'

No comments:

Post a Comment