Matt Neal ni kijana mwenye umri wa
miaka 26, akitokea Ann Arbor, Michigan huko Marekani aliwahi kutangaza
kuuza viatu vyake aina ya Yeezy 350 ambavyo ni mali kutoka kampuni ya
utengenezaji wa viatu inayomilikiwa na Mwanamuziki Kanye West.
Kijana huyu alihangaika sana kutafuta
matibabu bila mafanikio kutafuta matibabu ya ugonjwa wake wa figo na
kujikuta akiishiwa fedha kabisa hivyo akaamua kuanza kuuza vitu vyake
vya thamani, mavazi na viatu.
Sasa baada ya Kanye kupata habari hizo za mteja wake kuuza viatu ameamua kumlipia pair nyingine ya viatu kwa kijana huyo.
Kanye ambaye ametangaza kwamba huenda
akagombea urais wan chi ya Marekani mwaka 2020, amesema atampa kijana
huyo viatu vingine vipya kwa ajili ya kufidia hivyo anavyotaka kuviuza
kupata matibu ya matibabu ya figo.
No comments:
Post a Comment