Monday, 7 September 2015

Unafahamu chanzo cha Kondomu! Kisome hapa

                                                   
Kondomu ni kifaa/ zana iliyotengenezwa mahususi kuvalisha uuume au ukeni wakati wa kujamiiana. dk. condom alifahamika kama mgunduzi wa kwanza wa kondomu ambaye alikuwa ni daktari wa mfalme Charles II. Hivyo ndiyo alili ya neno “CONDOM”. Aidha, Dk. Condom alimshauri mfalme kutumia kama kinga kutokana na magonjwa ya zinaa kutokana na tabia yake ya kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa yake. Imeelezwa kuwa kondomu zipo za aina tofauti kutokana na muda na vipindi zilipotengenezwa.



AWAMU YA KWANZA

Kondom zilitengenezwa kwa mimea na zilikuwa mahususi kama kinga dhidi ya maambukizo ya vimelea vya ugonjwa wa kaswende “ugonjwa wa kifaransa”

AWAMU YA PILI

Zilitengenezwa kutokana na utumbo wa kondoo.

AWAMU YA TATU

Kutokana na mpira, hizi zilitengenezwa kuwa urahisi na kwa wingi na zikawa ndizo pekee zenye uwezo wa kudhibiti mimba hadi miaka ya 1960 vilipogunduliwa na vidonge vya majira. Hata hivyo, tafiti zimeonyesha kuwa kondomu haiina uwezo wa kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa vikiwemo virusi vya ukimwi kwa kiwango cha asilimia mia moja.

-Human Life International Tanzania

No comments:

Post a Comment