Friday, 11 September 2015
P Square walalamika video zao kutokuchezwa Sound City
Kundi bora la muziki, Barani afrika P-Square wameibuka na kuanza kutupa maneno ya lawama mitandaoni kuhusu kituo cha runinga nchini mwao Nigeria SoundCity kutokucheza Video zao.
Jana Kaka wa ndungu hao wanaounda kundi la P-Square Jude Okoye naye alikuja juu na kuwaunga mkono ndugu zake huku akitupa madongo kwa kituo hicho cha kurushia matangazo.
Hata hivyo SoundCity wameshangazwa na tuhuma hizo kwani ni miaka mingi walikuwa wakiwasapoti ndugu hao na kudai kwamba hakuna kituo kingine cha Runinga kilichokuwa kinacheza nyimba za P-Square kama CitySound.
Kwa mujibu wa P-Square tangu ajnuary mwaka huu kituo hicho hakija wahi kucheza video zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment