Monday, 7 September 2015
Zifahamu hatari katika uhusiano zitokanazo na wapenzi kufuatana kwenye mitandao ya kijamii
Ni kawaida kwa mtu kuwa rafiki wa mpenzi wake kwenye Facebook au kumfollow kwenye Instagram lakini mtaalam wa masuala ya mahusiano ameonya kuwa hiyo inaweza kuwa na athari kubwa.
Kwa mujibu wa Ian Kerner wapenzi ambao hawafuatani kwenye mitandao ya kijamii wana asilimia kubwa zaidi ya kuwa pamoja.
Mtaalam huyo mwenye makazi yake jijini New York amedai kuwa kuacha kumfuata mpenzi wako kwenye mitandao ya kijamii kunaweza kuimarisha zaidi uhusiano wako.
Amesema matumizi ya simu yanamaanisha kuwa wapenzi hutumia muda mchache kuzungumza ana kwa ana na hivyo kusababisha kutokuelewana na majibizano.
Kwa mujibu wa utafiti wa Pew Research Center, asilimia 25 ya watu walioana au kuishi pamoja wamewahi kuwatumia ujumbe wa simu wapenzi wao ilhali wakiwa pamoja ndani.
Idadi hiyo pia ilihisi kuwa wenza wao waliwahi kukerwa na simu zao na asilimia 8 wamewahi kubishana kuhusiana na muda wa wenzi wao wanaotumia mtandaoni.
Kerner, ambaye kwa sasa ameifuta akaunti yake ya Facebook amedai kuwa wakati alikuwa nayo naye pia alikutana na changamoto kadhaa kwenye ndoa yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment