Director wa Kwetu Studio Msafiri ambaye amerekodi ngoma mbalimbali ikiwemo ngoma ya ‘Sielewi’, ngoma za Hemed PHD..amesema
wameibiwa vifaa baada ya kuvamiwa wakiwa hotelini, wameiba camera, lens
pamoja na compyuta ambavyo gharama ni zaidi ya milioni 15.
Amesema walikua wakitengeneza kipindi kule Kisarawe na walivunja mlango wakati wakiwa kwenye kipindi.
Pia kulikuwa na video ambazo zimepotea ikiwemo ya
Hemed, msanii wa Arusha Mbaula pamoja na vipindi vya watu.
Pia kuna kazi za wasanii za siku nyingi ambazo zilikuwa bado hazijachukuliwa.
No comments:
Post a Comment