Mshambulizi raia wa Senegal, Pape
N’daw amekamilisha usajili wa Simba SC kuelekea msimu mpya wa ligi kuu
Tanzania Bara na michuano ya kombe la FA. Simba inataraji kuanza msimu
wa 2015/16 kwa kucheza na African Sport ya Tanga mwishoni mwa wiki
ijayo, na tayari imekamilisha usajili wa nafasi zote saba (7) za
wachezaji wa kigeni.
Simba imewasaini jumla ya
wachezaji 16 wapya huku idara ya mashambulizi akibaki kijana Ibrahim
Ajib pekee kutoka katika kikosi cha msimu uliopita. Wachezaji raia wa
Uganda, Hamis Kizza, Juuko Murshid, Simon Sserunkuma, Mrundi, Emiry
Nimubona, Mzibabwe, Justive Majabvi pamoja na golikipa raia wa Ivory
Coast, Vincent Angban wamesajiliwa kama nyota wa kigeni.
“Tunaweza kufikia malengo kutokana na kikosi tulichonacho” amesema kocha mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr.
Kikosi kamili ni kama ifuatavyo;
MAGOLIKIPA: Vincent Angban, Manyika Peter Manyika na Denis Richard.
WALINZI: Hassan Kessy, Hassan
Isihaka, Samih Hajji Nuhu, Abdi Banda, Mohamed Hussein, Juuko Murshid,
Mohamed Fakhi na Emiry Nimubona.
VIUNGO: Jonas Mkude, Said Ndemla, Justice Majabvi, Simon Sserunkuma, Peter Mwalyanzi, Mwinyi Kazimoto, Awadh Juma.
WASHAMBULIAJI: Musa Hassan
Mgosi, Daniel Lyanga, Ibrahim Ajib, Joseph Kimwanga, Boniface Maganga,
Issa Abdallah, Said Issa, Emanuel Mtumbuka, Hamis Kizza, Pape N’daw.
No comments:
Post a Comment