September 16 2015 nilikusogezea stori kuhusu ishu ya mtoto wa miaka 14, Ahmed Mohamed mwanafunzi wa MacArthur High School iliyoko Irving, Texas Marekani kukamatwa na Polisi baada ya kwenda na saa ambayo Walimu waliifananisha na Bomu !!
Ahmed aliibuni
saa hiyo yeye mwenyewe, lakini kutokana na muonekano wake Walimu
walishtuka wakijua kaibuka na Bomu Shuleni, good news ni kwamba hiyo
ishu imefika mpaka White House, Ikulu ya Rais Barack Obama Marekani.
Rais Obama ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter ujumbe wa kumkaribisha Ahmed ndani ya Ikulu ya White House,
kaonekana kuvutiwa na kipaji cha huyu mtoto na mwaliko huo kautoa kama
njia ya kufanya watoto wengi waipende Sayansi na kuwa wabunifu.
No comments:
Post a Comment