No comments
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2015/2016 inatazamiwa
kuanza kutimua vumbi jumamosi Septemba 12, 2015 kwa michezo saba
kuchezwa katika viwanja tofauti nchini.
Ndanda FC ya Mtwara watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja
wa Nagwanda Sijaona mjini Mtwara, Wana kimanumanu African Sports
watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku
Wana Lizombe Majimaji wakiwa wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu katika
uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Azam FC watakua wenyeji wa Tanzania Prisons kaika uwanja wa Chamazi
Complex, Stand United FC chama la wana watawakaribisha Mtibwa Sugar
katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto Africans
watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya City watacheza
na Kagera Sugar katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Jumapili Ligi Kuu itaendelea kwa mchezo mmoja tu utakaochezwa katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo mabingwa watetezi wa kombe
hilo Yanga SC watawakribisha wagosi wa kaya Coastal Union.
Katika hatua nyingine klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera
itatumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kwa mechi zake za
nyumbani dhidi ya Toto Africans (Sept 26), JKT Ruvu (Sept 30), Tanzania
Prisons (Oct 4) na Yanga (Oct 31).
Mabadiliko hayo yamefanyika kupisha shughuli ya uwekaji nyasi bandia
inayoendelea kwenye uwanja wao wa Kaitaba mjini Bukoba unaofanywa na
wataalamu kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
No comments:
Post a Comment