Thursday, 17 September 2015

DJ Fetty: Nilikuwa najua napendwa lakini si kwa kiwango hiki







DJ Fetty alijua kuwa anapendwa lakini si kwa kiwango alichokiona jana mara baada ya kutangaza kuwa anaacha kazi ya utangazaji kwenye kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kukitumikia kwa zaidi ya miaka 10.

Fetty atakumbukwa kwa utangazaji wake wa kipekee wa masuala ya burudani, uwezo wake mkubwa wa kuchambua hoja zinazohusiana na showbiz na ofcourse kicheko chake kilichowaacha hoi watu wengi. Yeye mwenyewe anasema huo ni uamuzi mgumu sana kuufanya.

“It’s the moment I will never forget in my life,” aliandika kwenye Instagram.

“Ni maamuzi magumu sana lakini maisha lazima yaendelee. Pole sana kwa wote niliowakwaza kwa uamuzi huu, lakini ni uamuzi niliouamua baada ya kufikiria na nimeamua mwenyewe kwa roho safi kabisa. Nimefanyakazi na @cloudsfmtz kwa miaka 10 sasa na ni familia ambayo sitaisahau kwa upendo walionao kwangu. I will definitely miss @bdozen sanaaaaaa he is the best of the best @adamchomvu I love u too mshkaji wangu to all my fans out there, got mad love for u. I’m here nipo sana tu na karibuni.”

“I will definitely miss u guys thanks once again for the love. Nilikuwa najua nakubalika but didn’t know is this much,” ameongeza Fetty kwenye post nyingine.

Ni habari iliyowasikitisha watu wengi kama vile wamempoteza mtu muhimu kwenye maisha yao. Si jambo la kushangaza sababu redio ni chombo chenye nguvu kubwa na kinachotengeneza ‘connection’ isiyoelezeka kati ya mtangazaji na msikilizaji.

Na kwakuwa redio ni chombo ‘personal’ mtangazaji anapokuwa hewani pamoja na kusikika na watu wengi kwa wakati mmoja, huongea na mtu mmoja binafsi.

Ndio maana mtangazaji huwa hasemi ‘mambo vipi wasikilizaji’, husema ‘mambo vipi msikilizaji’. Kwahiyo maana yake ni kuwa Fetty kama watangazaji wengine amekuwa na urafiki na msikilizaji mmoja mmoja kwa zaidi ya miaka 10. Kwahiyo nawaelewa kabisa wasikilizaji ambao habari ya yeye kuachana na utangazaji wameipokea kwa majonzi makubwa.

Hakuna anayebisha ukweli kuwa XXL ni kipindi cha mchana chenye mashabiki wengi sana Tanzania na kwa miaka mingi, B12, Fetty na Adam Mchomvu ndio wamekuwa ‘signature’ yake.

Kuondoka kwa Fetty kutatengeneza pengo ambalo naamini hakuna mtangazaji hata wa kike anayeweza kuliziba. Hii ni kwasababu tofauti na watangazaji wa kiume ambao wapo wengi wenye uwezo unaokaribiana, hakuna mtangazaji mwingine wa kike (kama yupo basi hajatusua) kwenye vipindi vya burudani katika redio unayeweza kumfananisha na Fetty.
Fetty ni mtangazaji aliyekuwa kwenye ligi yake mwenyewe na na hii ni kwasababu vipindi vingi vya redio hasa vya burudani huongozwa na wanaume.

Fetty amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye muziki wa Tanzania ambapo tofauti na XXL, kipindi chake cha So So Fresh nacho alikuwa akikitumia kuukuza muziki. Uwezo wake wa kufanya interview na kuuliza maswali ya msingi ni kitu kingine ambacho XXL na So So Fresh vitamiss sana.

“It is just a normal Tuesday to others but a sad Tuesday to the music, entertainment and broadcasting industry,” ameandika shabiki wake mkubwa aitwaye Kevarist kwenye Instagram.

“She has served for ten years. She has built confidence and influenced people from different walks of life with respect to broadcasting and handling entertainment activities at large. Regardless of her being a special friend and a sister to me I always tune to radio and listen to her special skills, maturity, great interviewing skills and undisputed talent behind the microphone. We will miss listening to your voice, qualities and even your laughter. The legacy you have left behind and the courage of deciding to be the first the first female Dj in the country will always prevail and inspire youngsters,” aliongeza.

“Fetty you r the bestest. I bet this country will take time to have your substitute. Trust me, history is written on 15th September, 2015. Salute Fetty. I am proud of you. Thanks for serving and for your tirelessly contribution to the industry.”

Naye rapper Black Rhyno ameandika: THE GAME WILL BE MISSING YOU. U have inspired many u have helped many into this game. But I wish you the best for your future.”

Mtangazaji mwenzake Diva ameandika: A very special Moment for @thebestfetty we gonna miss you Mami. all the best. we love you . Wish nothing but the best .. for you Boo, ilikuwa ni furaha kufanya kazi na wewe. learned a lot from you .We keep You closer.”

Kwa upande wake muimbaji wa Tanzania anayeishi Marekani, Erica Lulakwa amesema: Sometimes in life we choose to make tough choices; and that leads us to greater success. @thebestfetty thank you so very much for your work. You are the light to artists who were in darkness. I am honored to have been on your show back in 2012. You made @Tanzania @cloudsfmtz @bdozen and @adamchomvu proud. Keep the ball rolling.”

Vanessa Mdee ameandika: Fetty asante kwa mchango wako mkubwaaaaa kwenye hili game. Kila la Kheri on whatever comes next. God bless and guide you sister �� @thebestfetty #OntoTheNext #AirwaveQueen #KileKichekoSasa #StrongGirl.”

Naye producer wa AM Records, Bob Manecky ameandika: Your such a special person and we’ll miss your caring ways.. We’ll remember your sense of humor that got us through many days. We know You have a dream to follow and we are very excited for you. We hope you’ll enjoy your new life And be happy in all you do… #FarewellSissy.”

Fetty anadai anaenda kufanya mambo yake binafsi na kwakuwa tunajua amefungua duka la nguo lililopo chini ya kampuni yake Fettylicious Co.LTD, bila shaka ameamua kuwekeza nguvu zaidi kwenye kujiajiri mwenyewe. Suala la kama anaweza kurejea tena hewani kwenye kituo kingine cha redio au TV linabaki kuwa kwenye moyo wake mwenyewe lakini naamini kuna siku atarejea tena.
244


No comments:

Post a Comment