Kama kungekuwa na uwezo wa kutumia
Computer kupika chakula maisha yangekuaje? Au kama simu yako ingekuwa na
uwezo wa kupokea ujumbe wa kukutaarifu kuwa chakula chako kipo tayari
maisha yangekuaje!?
Nimekutana na stori kutoka Marekani ambako Matt Van Horn na rafiki yake Nikhil Bhogal wametengeneza computer waliyoipa jina ‘June Intelligent Oven’.
June ni oven ya computer inayofikiria na kufanya kazi kama mpishi ‘chef’, oven hiyo inayopatikana kwa dola 1,495 (Million 3,289,000) inatumia computer kutambua ni aina gani ya chakula unataka kupika na kukuelekeza jinsi ya kukipika vizuri zaidi.
>>“hili
oven lina uwezo wa kufanya kazi kama computer, simu au hata tablet… kwa
uraisi na ufupi ‘June’ ni computer yenye uwezo wa kupika chakula
chochote bila msaidizi au mpishi”.<<< Matt Von Horn.
Hili oven halhitaji kuwashwa ili likolee
moto lenyewe hufanya kazi kama vile computer nyingine na kizuri zaidi
ni kwamba kwa kutumia application yake ya simu iitwayo ‘June Application’ hili oven lina uwezo wa kutuma ujumbe mfupi kwenye simu yako kukutaarifu pale chakula chako kikiwa tayari!
Ni mwaka jana tu ambapo Matt na Nikhil waliamua
kuacha kazi zao ili kuifanyia kazi ndoto hii, na mwezi uliopita June
Intelligent Oven ilizinduliwa rasmi lakini jiko hilo litaanza
kusafirishwa mwanzo wa mwaka ujao.
Hizi ni baadhi ya picha za oven la June nilizoweza kuzinasa..
Na hapa chini nimekusogezea video yake ikielezea jinsi ya kutumia oven hio kwa kutumia simu au tablet yako mtu wangu.
No comments:
Post a Comment